Soko la Chuwini kuleta mapinduzi kiuchumi

ZANZIBAR: KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, CPA Amos Makalla amesema soko la kisasa la Chuwini litaleta Mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa wananchi Zanzibar.

Amesema hayo leo jana Januari 31,2025 alipokuwa akikagua mradio huo wa kimkakati kwenye muendelezo wa ziara yake ya mikoa sita ya kichama visiwani Zanzibar.

Amesema kuwa soko hilo kubwa zaidi ya soko la kariakoo jijini Dar es Salaam kwani litachukua zaidi ya Wafanyabiashara Elfu Nne kwa wakati mmoja ambapo lile la Kariakoo litachukua wafanyabiashara kati ya 3000-3500.

Aidha amepongeza ubunifu wa kuchanganya soko pamoja na kituo cha mabasi kwa itasaidia sana kukua kwa biashara.

“Nami nijumuike nanyi kuwa kuwapongeza Viongozi wetu dkt Samia na Dkt Hussein Mwinyi kwa namna wanavyoshirikiana katika kuwaletea maendeleo nilikuwa naona tu kwenye Mitandao nimejionea soko kubwa la kisasa kabisa na kubwa na kupitia hili nimeshawishika kwanini Wajumbe waliamua Dk Samia na Dk Mwinyi wawe wagombea wa urais Mapema”

“Kwani hapa mmeweka historia kutoka Bonde la mpunga mpaka soko la kisasa sasa wale Zambarau wenye miwani za Mbao waje wajionee kazi ilivyofanyika kwani kuona ni kuaminiā€ alisema

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button