Bolt yaleta huduma ya kumsaidia dereva,abiria

DAR-ES-SALAAM : KAMPUNI ya Bolt imezindua rasmi kipengele cha “Trusted Contacts” jijini Dar es Salaam, ambacho kitawawezesha abiria na madereva kuongeza majina na namba za simu za marafiki au ndugu kwenye orodha ya mawasiliano ya akaunti zao.
Kipengele hiki kitasaidia Timu ya Usalama ya Bolt kuwasiliana na majina yaliyoongezwa kwenye orodha ya mawasiliano, endapo mmiliki wa akaunti hawezi kupatikana.
Uzinduzi huu ni sehemu ya uwekezaji mkubwa wa Bolt katika kuboresha vipengele vya usalama kwenye jukwaa lake, ili kuhakikisha kuwa taarifa muhimu za Ride Check, maombi ya Emergency Assist, na matukio mengine ya usalama yanashughulikiwa kwa haraka endapo mmiliki wa akaunti hayupo kwenye mawasiliano.
“Trusted Contacts” inajiunga na vipengele vingine vya usalama vilivyopo kwenye programu ya Bolt, kama vile Ride Check inayobaini hali isiyo ya kawaida wakati wa safari, Share Location ambayo inawawezesha abiria kushiriki eneo lao kwa muda halisi na familia au marafiki, pamoja na Emergency Assist inayowawezesha abiria kutoa tahadhari ya dharura kwa vyombo vya usalama au washirika wa ulinzi binafsi kwa njia ya haraka na ya siri.
SOMA: Bolt waongeza nauli asilimia 10
Meneja Mkuu wa BoltĀ Tanzania na Kenya, Dimmy Kanyankole alisema, “kupitia Trusted Contacts, tunapanua juhudi zetu za kuhakikisha kuwa tukishindwa kumpata mwenye akaunti ya Bolt, tunaweza mara moja kuwasiliana na rafiki au mwanafamilia wake. Hili ni sehemu ya uwekezaji wetu wa kuimarisha usalama kupitia bidhaa na vipengele vipya pamoja na timu yetu ya usalama yenye mafunzo maalum.
“Lengo letu ni kuendelea kuboresha mfumo wa usalama wa Bolt ili kutoa safari salama na za kuaminika kwa madereva na abiria. Kwa kuendelea kuweka usalama wa abiria na madereva kuwa kipaumbele, uzinduzi wa Trusted Contacts ni hatua nyingine muhimu kuhakikisha safari salama na yenye kuaminika.



