Samia abariki ujenzi Makao Makuu CCM

DAR ES SALAAM; Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, ameweka jiwe la msingi, kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya CCM katika hafla iliyofanyika eneo la Tambuka reli, jijini Dodoma, litakapojengwa jengo hilo.

Uzinduzi huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi mbalimbali, wakiongozwa na viongozi na wanachama wa CCM, umefanyika leo Jumatano Mei 28, 2025.



