Watu 300 wapoteza maisha Pakistan

ISLAMABAD : IDADI ya vifo imefikia karibu watu 300 kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha kuporomoka kwa majengo katika Wilaya ya Buner, Kaskazini Magharibi mwa Pakistan.
Waokoaji wameendelea kuopoa miili kutoka kwenye vifusi, huku mashuhuda wakieleza kuwa bado kuna kadhaa hawajulikani walipo. Mafuriko hayo yalisababishwa na mvua kubwa zilizotiririka kutoka milimani, na kuathiri pia jimbo la Kashmir. SOMA: Mafuriko yaua 30 Nigeria