Bandari Dar yafikisha shehena milioni 27.76

DAR ES SALAAM: BANDARI ya Dar es Salaam imeongeza uwezo wa sheheza za mizigo kutoka tani milioni 17 mwaka 2020 hadi tani milioni 27.76 mwaka 2025.

Pia bandari hiyo imepunguza muda wa meli kutia nanga kutoka wastani wa siku 46 hadi siku 7 kwa meli za mizigo mchanganyiko.

Akizungumza leo Agosti 28, 2025 katika uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgombea urais wa chama hicho amesema pia meli za makasha zimepunguza muda kutoka wastani wa siku 10 hadi siku 3.

SOMA ZAIDI

Bandari ya Dar kuimarisha usafirishaji wa mazao

 

Akitaja mafaniko ya serikali katika sekta ya bandari, Rais Samia amesema idadi ya meli imeongezaka kutoka meli 1860 mwaka 2023 hadi 1900 mwaka 2025.

“Meli kubwa za tani 65 zimeanza kutia nanga Dar es Salaam ukilinganisha na meli za ukomo wa tani 45 kabla ya mwaka 2021,” amesema Rais Samia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button