Mpango asema Tanzania iko tayari kwa Uchaguzi Mkuu

MADAGASCAR : MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amesema maandalizi muhimu kwa ajili ya kufanya Uchaguzi Mkuu wa haki, uhuru na uwazi yanaendelea vizuri nchini na kutoa mwaliko kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutuma timu ya waangalizi kwenye uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Dk Mpango alitoa wito huo wakati anasoma hotuba ya ufunguzi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama jijini Antananarivo, Madagascar jana. Kiongozi huyo ambaye anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo alitaja mafanikio kadhaa ya uenyekiti wa Tanzania katika asasi hiyo, iliyopewa jukumu la kusimamia masuala ya ulinzi, amani na usalama katika kanda ya SADC.

Akibainisha mafanikio hayo, alieleza kuwa mwaka mmoja wa Rais Samia katika Asasi hiyo, eneo la SADC limesalia kuwa tulivu, isipokuwa Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambapo jitihada za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo zinaendelea. gogoro huo zinaendelea. Jitihada hizo ni pamoja na majadiliano kupitia Mpango wa Luanda na Nairobi na hatua zilizochukuliwa na Wakuu wa Nchi katika mikutano ya pamoja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na SADC.

Alisema kupitia mikutano hiyo jopo la Wazee wa Hekima kusuluhisha mgogoro huo limeundwa, timu za wataalamu kutoka EAC, SADC na Umoja wa Nchi za Afrika (AU) zimeunganishwa, zifanye kazi kwa pamoja, utaratibu na hadidu za rejea za namna ya kushughulikia mgogoro huo zimetayarishwa.

Dk Mpango alisisitiza umuhimu wa migogoro inayoibuka Afrika kutafutiwa suluhu na Waafrika wenyewe, kwa nchi hizo kuwa na dhamira ya dhati na kujitoa kwa hali na mali. Aliendelea kwa kueleza kuwa katika kipindi cha uenyekiti, Tanzania pia imeongoza programu zinahusu uzuiaji na usuluhishi wa migogoro, upelekaji wa vikosi vya kulinda amani kwenye maeneo ya machafuko ya kisisasa, uimarishwaji wa taasisi imara za kidemokrasia na kuongoza timu za waangalizi wa uchaguzi katika nchi za Botswana, Namibia, Mauritius na Msumbiji.

Alieleza Tanzania imejitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kanda ya SADC inasalia kuwa tulivu na salama na kuahidi kuwa nchi yake itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika kwa mwenyekiti mpya wa asasi hiyo ambayo ni Malawi. SOMA : Dk Nchimbi: Matiko ni silaha madhubuti kisiasa

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button