Wadau waipongeza serikali ubora huduma za afya

MOROGORO: WADAU wameipongeza serikali kwa kufanya uwekezaji mkubwa na uboreshaji miundombinu ya kutolea huduma za afya katika hospitali mbalimbali nchini ikiwemo uwekaji wa vifaa tiba vya kisasa kwa ajili ya magonjwa ya dharura.
Licha ya uboreshaji miundombinu ya kutoka huduma za afya Serikali imewezesha pia kuwepo kwa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ambao wamekuwa ni msaada mkubwa katika kuokoa maisha ya wananchi.
Mmoja wa Wakurugezi wa Kampuni ya Al Saedy, Assad Al Saedy ametoa pongezi hizo baada ya kukabidhi mashine mbili za kisasa za kuwasaidia watoto wagonjwa kupumua kwa urahisi haswa wenye kuzaliwa kabla ya muda (Continuous Positive Airway Pressure –CPAP) .
Saedy amesema kuwa kampuni yao inaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika sekta ya afya kwa kuchangia mashine hizo mbili ili kupunguza uwezekano wa kuongezeka vifo vya watoto wachanga na wale ambao hawajatimiza umri kutokana sababu za kiafya.
“Kama kampuni tukaona muhimu wa sisi kutoa mchango wetu baada ya kuguswa na kuwaletea hivi vifaa ili iendelee kuokoa maisha ya watoto ambao ni vizazi vyetu vya baadaye,” alisema Saedy.
“Tumeona tufanye hivyo na tutazidi kuendelea kutoa mchango na kuhamasisha wadau wengine kwa sababu ni budi tuokoe vizazi hivi ambavyo vitakujakuwa ni vijana wa baadaye wa taifa letu,” amesema.
Amempongeza Rais Dk Samia Suluhu Hasaan na Serikali yake kwa uwekezaji huo mkubwa kwenye sekta ya afya ambao umewezesha upatikanaji wa huduma Bora na za kisasa na kwa gharama nafuu kwenye hospitali zote za serikali.
Naye Daktari Bingwa wa Watoto wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo, Asha Bossy ameushukuru uongozi wa kampuni hiyo kwa kutoa mashine hizo ambazo zitasaidia kuokoa maisha ya watoto ambao bado hawajatimiza na wanaozaliwa kabla ya umri pamoja na watoto ambao wanakuwa na shida za kupumua .
“ Tumepata mashine mbili za CPAP zinasaidia watoto wanaoshindwa kupumua wanaozaliwa kabla ya siku vile vile zinasaidia watoto waliozaliwa vizuri wametimia siku isipo kuwa wana shida ya kupumua,”amesema Dk Asha.
Daktari Bingwa wa watoto huyo ametolea mfano kuwa mashine hizo zinasaidia kwa mtoto anayezaliwa kwenye mapafu yake yanakuwa na kitu kama mgando katikati kumwezesha kupumua.
Dk Asha amesema mashine hizo zinaumuhimu mkubwa kwa kuwa zitasaidia kuokoa maisha ya watoto hasa wale wachanga zaidi kuanzia siku saba na pia zitasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga.
“Kwa niaba ya hospitali ya mkoa, mganga mkuu wa mkoa mganga mkuu wa hospitali ya mkoa tunashukuru kwa hizi mashine “ amesema Dk Asha .
Dk Asha amesema hospitali ya Rufaa ya mkoa huo kwa sasa ina vifaa vya kisasa na mashine mbalimbali zikiwemo za kupunguza manjano kwa watoto ,madaktari wabobezi pamoja na wauguzi wabobezi .
Kwa upande Ofisa Muunguzi wa Kituo cha Uangalizi wa karibu,Dorice Nzengele anasema kuwa uhitaji wa mashine hicho za CPAP ni mkubwa kutokana na idadi ya wagonjwa wanaowahudumia kwa siku ni 7-12.
Nzengele amesema kuwa kati ya hao 4-6 ni watoto walio zaliwa kabla ya muda yaani premature na wenye changamoto ya upumuaji.
Amesema uwepo kwa wingi wa vifaa hivyo na vinavyoendelea kutolewa msaada wa wadau kumeweza kuleta mafanikio makubwa ya kuwaokoa watoto wachanga ambao wanazaliwa kufikia muda wao na wale wenye shida ya kupumua.
“Mfano kwa miezi kadhaa tumefanikiwa kuokoa maisha ya mtoto ambaye alizaliwa na gramu 500 na hata sasa unamfuatilia kwa mama yake amefikisha umri wa mwaka mmoja sasa anaendelea vizuri na wapo watoto wengine ambao wamezaliwa na gramu 650,”amesema Nzengele.
Google pays $300 on a regular basis. My latest salary check was $8600 for working 10 hours a week on the internet. My younger sibling has been averaging $19k for the last few months, and he constantly works approximately 24 hours. I’m not sure how simple it was once I checked it out.
This is my main concern……………………………. http://Www.Cash43.Com