CCM yaahidi stendi ya kisasa Mwanga

MWANGA, Kilimanjaro: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewaahidi wakazi wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, kuwa kikipata ridhaa ya kuwa madarakani miaka mitano ijayo, kitajenga stendi mpya kisasa katika eneo la Mwanga.
Hatua hiyo italenga kutatua changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa stendi katika mji huo.
Mgombea Mwenza wa Urais wa chama hicho, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amesema hayo leo katika viwanja vya Cleopa Msuya Mwanga akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Kauli hiyo iliibuka shangwe na vigelegele kwa wananchi wa eneo hilo ambao walisema ukosefu wa stendi imekuwa changamoto kubwa kwao sasa kilio chao kimesikika.



