Marekani yadhibiti sheria za TikTok

WASHINGTON DC : SERIKALI ya Marekani imetangaza kuwa makampuni ya Marekani yatadhibiti mchakato wa kanuni za kompyuta (algorithm) za TikTok nchini humo kupitia mkataba mpya unaotarajiwa kusainiwa na China.
Waziri wa Vyombo vya Habari, Karoline Leavitt, amesema makubaliano hayo yanaweza kusainiwa katika siku zijazo ingawa Beijing bado haijatoa tamko rasmi. SOMA: TikTok yapata mnunuzi, majina yahifadhiwa
Marekani imekuwa ikishinikiza kampuni mama ya TikTok, ByteDance, kuondoa ushiriki wake katika shughuli za programu hiyo nchini Marekani kwa sababu za usalama wa taifa. Hapo awali, TikTok iliagizwa kuuza shughuli zake au kukabili hatari ya kufungiwa.
Hata hivyo, Rais Donald Trump amechelewesha mara nne kutekeleza marufuku hiyo tangu Januari na wiki hii ameongeza muda hadi Desemba. Leavitt alisema usimamizi wa data na faragha za watumiaji wa Marekani utaongozwa na kampuni kubwa ya teknolojia, Oracle, inayoongozwa na bilionea Larry Ellison.



