Bandari Mtwara yapokea mafuta kwenda nchi jirani

BANDARI ya Mtwara imeanza kupokea meli zenye mzigo wa mafuta ambayo husafirishwa kwenda Zambia, Malawi na Burundi.

Meneja wa Bandari hiyo Ferdinand Nyathi amesema hayo leo wakati wa hafla ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja 2025.

SOMA: Bandari Mtwara yaendelea kuhudumia mizigo

“Bandari ya Mtwara imeendelea kufanya vizuri kibiashara na sasa hivi tumeanza kuhudumia mzigo wa ‘transit’ wa mafuta yanayokwenda kwenye nchi za Zambia, Malawi na Burundi,” amesema.

Meneja huyo amesema meli hizo zimeanza kuja mwezi wa tisa na mwezi huu na kushusha mzigo wa mafuta hayo  ambapo kipindi cha nyuma, hapakuwa na huhuduma meli ya mafuta kusafirisha kwenda nchi jirani kwenye Bandari ya Mtwara.

“Kwa hiyo mnaweza mkaona kuwa mwanga ni mkubwa kwenye kukua kwa Bandari ya Mtwara,” amesema na kuwashukuru watumiaji pamoja na wadau wa Bandari kwa kuendelea kuitumia bandari hiyo na kuifanya kukua zaidi.

Nyath amesema usafirishaji wa mizigo katika Bandari ya Mtwara imekuwa kwa kasi ambapo kwa sasa imefikia tani milioni 2.5 kwa mwaka 2024/25 kulinganisha na miaka minne nyuma ilipokuwa inasafirisha mizigo tani 500,000 kwa mwaka.

 

Habari Zifananazo

4 Comments

    1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
      .
      HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

    2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button