Watakiwa kutumia mitandao kwa busara

MWENYEKITI wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere, Paul Kimiti, amewataka baadhi ya viongozi na wanasiasa kuwa waangalifu katika matumizi ya mitandao ya kijamii, ili kulinda amani na mshikamano wa Taifa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Daily News Digital jijini Dar es Salaam, Kimiti amesema misingi ya uongozi iliyoachwa na Mwalimu Nyerere, inasisitiza matumizi ya busara na hekima katika kushughulikia changamoto za kitaifa, badala ya kutumia majukwaa ya mitandao kujibizana au kulaumiana. “Mwalimu alichukia mambo mawili; usije ukabishana juu ya jambo ambalo huna uhakika nalo, na pili, usishiriki mjadala usio na maana kwa sababu unaweza ukakuingiza katika upuuzi.

Pia, usizungumzie jambo bila kufanya utafiti wa kutosha,” amesema Kimiti. Amesema kuwa viongozi wanapaswa kuenzi falsafa ya Mwalimu Nyerere ya kusikiliza, kujadiliana kwa hoja zenye tija na kuheshimiana, ili kuendelea kulinda umoja na utulivu wa taifa. SOMA: Samia ataja ajenda tatu kuongoza nchi

Kwa mujibu wa Kimiti, taasisi anayoiongoza itaendelea kuelimisha jamii juu ya misingi hiyo, ikiwemo maadili, uwajibikaji, na busara katika mawasiliano ya umma. “Misingi hiyo ndiyo iliyojenga taifa letu. Tunapaswa kuilinda na kuienzi kwa vitendo, hasa katika kipindi hiki ambacho teknolojia ya habari inakua kwa kasi,” alisisitiza.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button