UTPC, IMS wachochea uandishi wa habari wenye tija

Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF), Dastan Kamanzi, ametoa wito mzito kwa waandishi wa habari nchini kujikita katika uandishi wenye tija, unaochochea uwajibikaji na maendeleo ya wananchi, akisema huo ndio uandishi unaojenga taifa lenye uwazi na haki.

Akizungumza mkoani Iringa kwenye mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na International Media Support (IMS), Kamanzi alisema TMF inataka kuona mageuzi makubwa ya namna waandishi wa habari wanavyoandika habari, ili vyombo vya habari virejee katika nafasi yake ya kuwa macho na sauti ya wananchi.

“Tunataka uandishi unachimbua na unaogusa maisha ya watu, unaouliza maswali magumu na kuchochea uwajibikaji wa viongozi ili kujenga taifa lenye maendeleo,” alisema.

Alisema TMF itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuboresha ubora wa maudhui ya habari nchini kupitia mafunzo, ruzuku za miradi ya habari na ufuatiliaji wa kazi za waandishi wanaoshiriki kwenye programu hizo, ili kuhakikisha maudhui yao yana matokeo halisi kwa jamii.

Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo ambayo mbali na kushirikisha waandishi wa habari kutoka ndani na nje ya mkoa wa Iringa wamewataka wanahabari kuacha uandishi wa “uchawa” na badala yake kusimamia misingi ya taaluma, ukweli na uwajibikaji.

“Kuna wimbi jipya la waandishi machawa—wanaoandika kwa upendeleo au maslahi binafsi. Huu si uandishi unaosaidia jamii. Mnapaswa kurejea kwenye misingi ya taaluma yenu: kuuliza maswali magumu, kuibua hoja zenye uzito na kusimamia ukweli bila woga,” alisema mmoja wao.

Naye Shani Nicolous wa Shamba FM alisema mafunzo hayo yamempa uelewa wa umuhimu wa kuandika habari zenye suluhu kwa jamii, huku Hakimu Mwafongo wa IPC akisisitiza wajibu wa wanahabari kutumia kalamu zao kutenda haki kwa wananchi.

Mwakilishi wa wadau wa habari, Raphael Mtitu, alisema wanatarajia kuona matokeo ya moja kwa moja kutokana na mafunzo hayo.

“Tunataka kuona mabadiliko kwenye maudhui—habari zenye suluhu, zinazogusa wananchi na kuchochea maendeleo. Huo ndio uzalendo wa kweli,” alisema Mtitu.

Naye Victor Maleko kutoka UTPC alisema mafunzo hayo yamelenga kuwaunganisha waandishi na jamii wanayoihudumia, ili habari zinazozalishwa ziwe na uhusiano wa moja kwa moja na maisha ya wananchi.

“Tafiti zinaonyesha sehemu ya jamii imeanza kupoteza imani na vyombo vya habari kutokana na kupungua kwa habari za uchunguzi na zinazochochea mabadiliko. Tunataka hali hiyo ibadilike,” alisema Maleko.

Mafunzo hayo ni sehemu ya programu endelevu za UTPC na IMS, zinazotekelezwa katika mikoa mbalimbali nchini, zikiwa na lengo la kuimarisha ubora wa vyombo vya habari na kukuza uandishi wa uwajibikaji ili kurejesha imani ya wananchi kwa wanahabari.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button