Mwinyi afurahishwa na biashara Darajani

MGOMBEA wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema lengo la Serikali ni kuendelea kuliimarisha eneo la Darajani na kujenga miundombinu zaidi ili wafanyabiashara wapate maeneo mazuri na ya kisasa ya kufanyia biashara.
Dk. Mwinyi ameeleza kuridhishwa na hali ya ufanyaji biashara katika eneo hilo, akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya wafanyabiashara ili kukuza uchumi wa wananchi na wa Taifa kwa ujumla.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 16 Oktoba 2025, alipokutana na wafanyabiashara na wajasiriamali wa soko la Darajani, ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa kampeni zake za kuomba kura na kuzungumza na makundi mbalimbali ya wananchi.
Amesema Serikali imepanga pia kujenga maegesho katika eneo la Malindi ili kuondoa utaratibu wa kuegesha magari kiholela. Aidha, ameeleza kuwa mradi mkubwa wa BIG Z, utakaojenga maduka pembezoni mwa barabara, unakuja na utaongeza haiba na mvuto wa eneo la mjini.
Akizungumzia barabara ya Malindi hadi Mnazi Mmoja, amesema itapanuliwa kuwa ya njia nne sambamba na ujenzi wa maegesho mapya katika eneo la Malindi.SOMA: Wafanyabiashara wahimizwa kutumia bandari Tanzania
Rais Dk. Mwinyi amesema kuwa katika awamu ijayo, Serikali itatenga fedha zaidi kwa ajili ya mikopo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali, hasa wale waliowahi kukopa na kurejesha mikopo yao kwa wakati, ili kuwaongezea mtaji na nguvu ya kiuchumi.
Kuhusiana na kodi, Dk. Mwinyi amesema Serikali itakaa na Chama Cha Mapinduzi kujadiliana juu ya namna bora ya kutatua changamoto hizo na kuona uwezekano wa kupunguza kodi kwa wafanyabiashara. Pia, ameliagiza Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kuweka transfoma mpya katika eneo la Darajani ili kumaliza tatizo la umeme linalowakabili wafanyabiashara.
Kwa upande wao, wafanyabiashara wa Darajani Souk wamemshukuru Dk. Mwinyi kwa mageuzi makubwa yaliyofanyika katika eneo hilo, ikiwemo kuboreshwa kwa mazingira ya biashara, kurejeshwa kwa kituo cha daladala na kuboreshwa kwa bustani, hatua zilizosaidia kuongeza idadi ya wanunuzi.
Wamesema wanathamini jitihada za Dk. Mwinyi katika kubadilisha sura ya Zanzibar na kuwajali wafanyabiashara wadogo na wa kati, huku wakiahidi kuendelea kumuunga mkono katika juhudi zake za kuleta maendeleo endelevu nchini.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com