Usalama wakwamisha wakimbizi DRC kurudi kwao

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limesema kuwa wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wanaohifadhiwa kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani ya Kasulu mkoani Kigoma hawataweza kurudishwa nchini kwao kwa sasa kutokana na maeneo wanayotoka kuwa na hali mbaya ya usalama.
Mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini, Barbara Bentum Dotse akizungumza kwenye mkutano na wakimbizi wa DRC kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Kasulu alisema kuwa shirika hilo haliko tayari kuwarudisha wakimbizi hao kutokana na hali mbaya ya usalama iliyopo kwenye maeneo hayo ambapo vita ya wenyewe kwa wenyewe inaendelea
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa UNHCR itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi hao hivyo limetoa wito kwa wakimbizi hao kuishi kwa kufuata sheria na taratibu za kuishi kambini hapo zilizowekwa ili kuepuka kuvunja sheria.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi ya Wizara ya Mambo ya Mdani ya Nchi, Sudi Mwakibasi alisema kuwa kutoweka kwa amani katika maeneo yao kutokana na migogoro ya kijamii na kisiasa ndiyo iliyowafanya wakimbizi hao kukimbia nchi yao na kukimbilia nchini na hali hiyo bado inaendelea hivyo wakimbizi hao hawataweza kurudishwa kwao katika hali hiyo.
Aidha, mkurugenzi huyo wa idara ya wakimbizi amewataka wakimbizi hao wa DRC kuishi kambini humo kwa kuzungumzia masuala yanayohusu amani badala ya mambo yanayowapelekea kuvunja sheria na kwamba Amani itakaporejea taratibu za kuwarudisha nchini kwao zitatekelezwa.
I’m making over $25,000 a month working part-time. I kept hearing other people talk about how much money they were making online, so I decided to look into it. Well, it’s all true and has completely changed my life. This is what I do. Check it out by visiting the following link:
COPY THIS →→→→ http://Www.Work99.Site
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com