BSS 16 yazinduliwa mshindi kupata mil 50

MSIMU wa 16 wa tamasha la Bongo Star Search (BSS) Next Level Revolution umeanza rasmi kuandaliwa, ukitarajiwa kuanza Novemba 22, 2025, mkoani Mwanza katika ukumbi wa La Kailo Hotel. Mshindi wa kwanza wa msimu huu ataondoka na Shilingi milioni 50 pamoja na gari jipya, akiongeza motisha kwa washiriki kushindana kwa bidii.
Akizungumza na Habari Leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa shindano, Madam Rita Paulsen, amesema kuwa msimu huu utakuwa wa kipekee kwa kuangazia vipaji mbalimbali ikiwemo uimbaji, uchoraji, sarakasi, uchekeshaji, upigaji vyombo na uchezaji. “Nimesimama kwa heshima kubwa na furaha isiyoelezeka kutambulisha rasmi msimu wa 16 wa Bongo Star Search,msimu mpya wenye sura mpya, nguvu mpya na dira mpya,” amesema Madam Rita.
Aidha, alitangaza ushirikiano wa kimkakati kati ya Benchmark 360 na Azam Media, ambao aliuona kama “ndoa ya maono” ya kukuza na kuangaza vipaji vya Afrika Mashariki na Kati kupitia jukwaa la BSS. Madam Rita alisema kuwa washiriki watatoka ndani na nje ya Tanzania, ikiwemo nchi za Kenya, Uganda, Congo, Malawi, Rwanda na Burundi.
Kwa Tanzania, mchujo wa awali utafanyika katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam kuanzia Novemba 22 hadi 23 (Mwanza) na Novemba 29 hadi 30 (Arusha). SOMA: BSS kufanyika Februari 28 Dar es Salaam
Kwa upande wake, Afisa Mwendeshaji wa Maudhui na Utangazaji wa Azam Media, Yahya Mohamed, alisema shindano hilo ni sehemu ya dhamira ya Azam Media kuendelea kutoa burudani bora kwa jamii. “Bongo Star Search Next Level Revolution ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuhakikisha burudani inawafikia Watanzania popote walipo,” amesema Yahya.
Shindano hilo litarushwa mubashara kupitia chaneli ya Sinema Zetu kwenye ving’amuzi vya Azam kila Jumapili saa 3 usiku, likiwa ni fursa ya kipekee kwa mashabiki kufuatilia kwa karibu vipaji vya kizazi kipya.




Online work turned out to be better than I imagined. Only 2 hours daily and I earned $18,542 in a month. Learn more here https://dailycash21.blogspot.com/
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website
Open This…. https://Www.Work99.site
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Hey you guys I have found the perfect job as a full time student, it has changed my life around! If you are self motivated and social media savvy then this is ideal for you. 22 The sky is the limit, you get exactly how much work you put into to it.
Click on this link to get started and
see for yourself………… https://Www.Smartpay1.site