Makonda aeleza mafaniko ya nchi sekta mbalimbali

SERIKALI imefanya maboresho katika sekta na maeneo sita mbalimbali kwa ajili ya kuchochea kasi ya maendeleo ya taifa na mwananchi mmoja mmoja.
Maeneo hayo sita ni bandari,nishati,utalii,Reli ya kisasa (SGR),miundombinu ya barabara kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na kilimo.
Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Arusha Mjini,Paul Makonda alisema hayo jana wakati akizungumza mkoani Mwanza.
Alisema serikali imejenga shule,madarasa na kukarabati miundombinu ya elimu kwa ajili ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu bora na yenye usawa.
“Serikali imefanikiwa kujenga shule za msingi 2,783 na sekondari zaidi ya 1,366, huku bajeti ya elimu ikiongezeka kutoka Sh bilioni 627 hadi kufikia Sh Trilioni 1.36,”alisema Makonda.
Alisema kwenye sekta ya kilimo serikali imefanya mageuzi makubwa kwenye kilimo na uvuvi, hatua inayodhihirisha dhamira yake ya kulifanya taifa liwe na uhakika wa chakula na kuongeza kipato kwa wananchi.
Alieleza kuwa serikali imeongeza bajeti ya sekta ya kilimo kutoka Sh bilioni 294 hadi kufikia Sh trilioni 1.22, jambo lililochangia kuongezeka kwa kasi kwa kilimo cha umwagiliaji na upatikanaji wa chakula cha kutosha nchini.
Alisema kutokana na maboresho hayo wakulima wanapata pembejeo kwa wakati,pia fedha zilizowekwa katika Benki ya Kilimo zimeongezeka kutoka Sh bilioni 60 hadi bilioni 4,44.Kupitia Ongezeko hilo vyama vya ushirika vimendelea kukopa kwa ajili ya mazao kama kahawa na pamba.
Makonda alisema katika sekta ya uvuvi,serikali iliwapatia wavuvi boti za kisasa na kuwawezesha kupata mikopo isiyo na liba inayotolewa na Benki ya Kilimo kwa ajili ya kupata vifaa vya kisasa vya uvuvi, hatua inayochochea maendeleo ya sekta hiyo na kuinua maisha ya Watanzania.
Alisema serikali imefanikiwa kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya maji, hatua inayoendelea kuboresha maisha ya Watanzania mijini na vijijini.
“Kwa sasa maeneo ya mijini yana uhakika wa upatikanaji wa maji kwa asilimia 91.6, huku vijijini huduma hiyo ikipatikana kwa zaidi ya asilimia 83,juhudi hizo ni uthibitisho wa dhamira ya serikali ya kuhakikisha hakuna mama anayeteseka kutafuta maji,”alisema.
Katika sekta ya afya Makonda alisema serikali imewahakikishia Watanzania upatikanaji wa huduma bora za tiba kwa watu wote kwa sababu afya ni moja ya maeneo muhimu katika ustawi wa taifa.
“Nimetazama sekta ya afya ambayo ni sekta muhimu sana katika taifa letu, kwakweli serikali imefanya mapinduzi makubwa,watanzania mnakumbuka tulikuwa na usumbufu mkubwa wa watu kupata huduma za upasuaji imetutoa kwenye vyumba vya upasuaji 388 na kutupeleka kwenye 577,” alisema.
Aidha, Makonda aliongeza kuwa watoto waliozaliwa katika mazingira magumu au wenye changamoto za upumuaji walikuwa na vyumba 80 pekee vya upasuaji, lakini serikali imejenga vyumba vingine 362, hatua iliyosaidia kuokoa maisha ya watoto wengi zaidi.




Nếu anh em nào mê thể loại nội địa thì nên ghé viet69, tốc độ xem ổn định, hình ảnh nét và gần như không có quảng cáo.
I’m making over $25,000 a month working part-time. I kept hearing other people talk about how much money they were making online, so I decided to look into it. Well, it’s all true and has completely changed my life. This is what I do. Check it out by visiting the following link:
COPY THIS →→→→ http://Www.Work99.Site
Begin now earning every month an extra amount of $17k or more just by doing very simple and easy online job from home. I have received $18953 in my last month direct in my bank acc by doing this easy home base job just in my part time for 2 hrs maximum a day online. Even a child can now do this job and earns money online. Everybody can get this home job right now and start earning dollars online by follow details here……….
Click the link—↠ https://www.Homeprofit1.site
I am making effectively tirelessly $15k to $20k basically by doing coordinate work at domestic. Multi month once more i have made $45890 from this development. astounding and smooth mac to do work and standard pay from this can be stupefying. i have propose each last one of you to connect this advance right specifically as moo security and get than full time compensation through take after this affiliation.
:
) AND Great Good fortune.:
)
HERE====)> https://cashprofit7.site