Tafiti 128 kutumika kusaidia wafanyabiashara

TAFITI 128 zilizolenga mada ya biashara na uchumi himilivu kwa ajili ya maendeleo jumuishi nchini Tanzania na nchi zinazoizunguka zimewasilishwa katika Mkutano wa sita wa Kitaaluma ulioandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).

Tafiti hizo zimetoa suluhisho kwa changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wafanyabiashara hususani wafanyabiashara wadogo.Hayo yalibainishwa jijini Dodoma na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Edda Lwoga wakati wa kuhitimisha mkutano huo.

Amesema mawasilisho hayo ni kutoka kwa watafiti wa ndani kutoka Chuo cha CBE na taasisi za elimu za juu hapa nchini pamoja watafiti kutoka vyuo vikuu kutoka nchi za Ethiopia, Finland, Uingereza, China na Afrika Kusini.

Amesema tafiti zilizowasilishwa zimetoa suluhisho kwa changamoto mbalimbali ambazo wafanyabiashara wanakutana nazo hususani wafanyabiashara wa chini ili waweza kukua na baadaye waweze kuwa wafanyabi ashara wa kati na juu.

“Tumeweza kusikia tafiti mbalimbali ambazo zinaangazia kwenye mada ya biashara na uchumi himilivyo kwa maendeleo jumuishi na kutoa suluhisho kwa changamoto za wafanyabiashara. Hivyo tunatarajia matokeo ya hizi tafiti yataenda kuwakwamua mwananchi kiuchumi ili yeye aweze kuchangia katika kukuza pato la taifa na kuendeleza nchi yetu,” alisema.

Aidha, Profesa Lwoga alisema baada ya kukamilika kwa kongamano hilo, chuo kitatengeneza muhtasari wa sera ambao utawasilishwa kwenye mamlaka husika ili iweze kusaidia katika kutunga miongozo mbalimbali katika sekta ya biashara na uchumi. “Kwa hiyo tunaamini mawasilisho haya yanaweza kuchangia kwenye utungaji wa sera na katika kutoa suluhisho kwa wananchi kwa kuangalia biashara zipi wafanye katika kutunga miongozo mbalimbali,” alisema.

Tangu mwaka 2019 CBE ilianza kongamano la kwanza la kimataifa la kitaalamu katika biashara na uchumi, tayari mawasilisho ya taifiti zaidi ya 480 yamewasilishwa ambayo yamekuwa yakichangia katika utungwaji wa sera na miongozo mbalimbali kwenye sekta ya biashara na uchumi. SOMA: TRA kulinda biashara binafsi

Awali, akiwasilisha mada kuhusu kujenga ujuzi, utamaduni na misingi ya kitaasisi kwa maendeleo endelevu, Dk Donath Olomi amesema kuwa na taasisi imara kutahakikisha utulivu na kuendeleza maendeleo ikiwemo sheria na sera zinazofaa pamoja na muundo wa kitaasisi unaoendana na malengo ya maendeleo.“Maendeleo endelevu yanahitaji kuelewa muktadha wa kijamii, kiutamaduni, na kisiasa ambao hauwezi kupimwa tu kwa takwimu,” alisema Dk Olomi.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button