Mfanyabiashara Pedima aendelea kung’ara ubunifu, uongozi

DAR ES SALAAM: Mfanyabiashara, Peter Mallya maarufu kama PEDIMA, ameendelea kuibua mvuto mkubwa katika tasnia ya biashara nchini kutokana na ukuaji wa kasi wa kampuni zake pamoja na mchango wake katika sekta za kifedha, teknolojia, afya na ajira kwa vijana.
Katika tuzo zilizotolewa jana na Naibu Waziri wa Madini,Dk Steven Kiruswa jumla ya washindi 50 walipata tuzo hizo huku Mallya akiondoka na tuzo mbili.
Mallya ambaye ni muanzilishi wa kampuni ya Pedima Enterprises, Pedima Microfinance, Pacify Limited na LocalPesa Limited,alisema katika utendaji kazi wake amejiimarisha katika kuleta mageuzi ya kidijitali na kutoa huduma bunifu zinazolenga kuboresha maisha ya Watanzania.
Akizungumzia safari yake ya ujasiriamali na maono yake kwa taifa, PEDIMA alisema anaamini katika kujenga kampuni za Kitanzania zenye uwezo wa kushindana kimataifa huku akisisitiza kuwa dhamira yake ni kuongeza usawa wa kifedha, nafasi za ajira na kukuza kizazi kipya cha wafanyabiashara nchini.
“Ninaamini katika kujenga kampuni za Kitanzania zenye uwezo wa kushindana kimataifa. Lengo langu ni kuongeza usawa wa kifedha, nafasi za ajira, na kukuza kizazi kipya cha wafanyabiashara nchini,” alisema.
Alisema kupitia kazi zake ataendelea kutoa mchango mkubwa katika jamii kupitia ubunifu unaolenga kutoa suluhisho kwa changamoto mbalimbali za wananchi.
Alieleza kuwa ataendelea kuboresha utendaji kazi wa kampuni yake ya Pacify inayongeneza bidhaa za afya ikiwemo Pacify Organic Pads, zinazotoa suluhisho salama, bora na nafuu kwa wanawake
Katika kipindi cha miaka michache,Mallya kupiyoa kampuni zake za PEDIMA ametwaa tuzo mbalimbali za ndani na kimataifa, zikiwemo 2023 FOYA Founder of the Year Under 30; 2024 Africa Company of the Year Awards (Company to Watch of the Year); 2024 CEO Top 100 Awards (CEO of the Year); 2025 Africa Company of the Year Awards (Fintech Company of the Year); 2025 Global Recognition Award Winner; na 2025 CEO Top 100 Awards (CEO of the Year – mara ya pili).



