Mamlaka ya maji yadai bilioni 4.2/- kwa wateja

TABORA: MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Tabora (TUWASA) inadai wadau wa huduma ya maji Sh bilioni 4.2 kutokana na kutoa huduma hiyo kwa taasisi za umma na watu mbalimbali mkoani humo.

Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Mayunga Kashilimu alisema hayo wakati wa uzinduzi wa baraza la sita la wafanyakazi wa Tuwasa.

Alisema kutokana na kuwepo kwa fedha nyingi nje zikidaiwa na mamlaka hiyo, shughuli nyingi zinakwama kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma za maji kwa wananchi.

Mayunga alimweleza Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Upendo Wella kwamba fedha hizo zilizo nje ni nyingi, hivyo ni muhimu kwa serikali kuangalia namna taasisi zitalipa fedha hizo.

“Tuomba serikali ione jinsi gani fedha hizo wanalipa kutokana na kubaki nje na wakizipata, waendelee kutoa huduma kwa watu wengine wenye mahitaji ya maji mkoani humo,” alisema.

Alisema Tuwasa inasambaza huduma za maji na zinakwenda katika wilaya za Urambo, Sikonge, Kaliua na Uyui mkoani hapa.

Alisema licha ya kutoa huduma za maji katika wilaya hizo, kumekuwa na changamoto ya wizi wa maji. Wella aliwataka watumishi katika sekta za umma kuwa na lugha rafiki wakati wa kuwahudumia wananchi na kutoa huduma kwa wakati na ufanisi. Aliwataka kupambana na wateja wasio waaminifu wanaohujumu mamlaka hiyo kwa kujiunganishia maji kwa njia za udanganyifu

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button