Abdul Nondo ajiandikisha daftari za mkazi

MWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, Abdul Nondo leo Oktoba 20 amejiandikisha katika daftari la mkazi kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Kiongozi huyo amejiandikisha katika mtaa wa Livingstone, kata ya Kasingirima, jimbo la Kigoma Mjini, Mkoa wa Kigoma.

Advertisement

Katika mazungumzo yake mara baada ya zoezi hilo, Nondo amewahimiza vijana wote nchini ambao bado hawajajiandikisha kujitokeza na kufanya hivyo leo. Zoezi la uandikishaji linafikia tamati leo.