Abiria bodaboda wasiovaa kofia wakamatwe

SHIRIKISHO la madereva wa pikipiki na bajaji, Dar es Salaam, limependekeza abiria wanaopanda pikipiki zaidi ya mmoja ‘mishikaki’ na wasiovaa kofia ngumu wakamatwe na kuchukuliwa hatua kwa kuvunja sheria kama ilivyo kwa madereva.

Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Said Chenja ameyasema  hayo leo Aprili  18,2023 wakati wakitoa mapendekezo yao mbele ya Tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini.

Chenja amesema sheria inakataza pikipiki maarufu bodaboda kubeba abiria zaidi ya mmoja pamoja na bajaji kubeba abiria zaidi ya watatu na anayekamatwa na kuwajibishwa kwa kosa hilo ni dereva pekee hivyo, ni wakati wa kuwawajibisha na abiria kwa kuwakamata na kuwaweka mahabusu.

Advertisement

“Kuna uvunjaji wa haki katika ukamataji, polisi anapomkuta dereva amepakia mishikaki anamkamata yeye tu na kumuacha abiria hii si sawa, wote wanapaswa kuwajibika,” ameeleza Chenja.