ACT Wazalendo: Asante babu Duni

VIONGOZI mbalimbali wa Chama cha ACT Wazalendo wakiwemo na kiongozi wa chama hicho,  Doroth Semu, mwenyekiti wa chama taifa ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Otham Masoud Othman, Makamu Wenyeviti wa Bara na Zanzibar, Katibu Mkuu na Manaibu Katibu wakuu jana wameshiriki halfa ya kumuenzi mwenyekiti mstaafu Juma Duni Haji kwa kazi alizofanya tangu mwaka 1992.

Mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo akipokelewa mara baada ya kuwasili ukumbi wa Majid Hall kwa halfa ya kumpongeza kwa utumishi wake.

Kiongozi Mstaafu wa ACT , Zitto Kabwe akimpokea na kumsalimia kiongozi wa chama hicho, Doroth Semu alipowasili kushuhudia halfa ya kumpongeza mwenyekiti mstaafu Juma Duni Haji.

Mwenyekiti wa chama taifa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Otham akiwa na mkewe kushoto wamemkabidhi zawadi pamoja na samani za ofisi Juma Duni kwenye halfa ya kumuaga.

Tukio hilo sehemu ya ACT Wazalendo kutimiza Sera mpya ya chama hicho ya kuwaenzi wastaafu.

Pamoja na zawadi nyingine chama cha ACT Wazalendo kimemkabidhi Juma Duni Haji gari mpya ya kutembelea kama moja ya takwa kwenye sera hiyo.

Baadhi ya wanachama wa ACT Wazalendo wakisherekea maisha ya utumishi ya Juma Duni Haji

Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu akielezea Sera ya Kuwaenzi viongozi wa staafu wa ACT Wazalendo.

Naibu Mwenezi wa Chama cha ACT Wazalendo, Shangwe Ayo akisoma tuzo ya heshima ambayo Sekretarieti ya Chama Taifa ili mkabidhi Mwenyekiti Mstaafu , Juma Duni Haji.

Kiongozi wa Chama, Doroth Semu akimkabidhi funguo ya gari Mwenyekiti Mstaafu kwenye hafla ya kumuaga jana.

Mwenyekiti Mstaafu akifurahi baada ya kukabidhiwa gari na chama hicho.

Naibu Katibu Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Nassoro Mazrui akimkabidhi zawadi mwenyekiti mstaafu Juma Duni Haji.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa ACT, Bonifasia Mapunda akikabidhi zawadi kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa ACT na Waziri wa Viwanda na Biashara, Omary Said Shabaan.

Makamu Mwenyekiti Zanzibar Ndunguru Ismail Jussa akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Msoud kwenye halfa ya kumpongeza Juma Duni Haji.

SOMA: SERA YA CHAMA YA KUWAENZI VIONGOZI WASTAAFU

Habari Zifananazo

Back to top button