ACT Wazalendo wataka mikakati zaidi ajira kwa vijana

DAR ES SALAAM: CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema serikali inapaswa kuweka nguvu zaidi kwenye suala la ajira kwa vijana, ili kuimarisha huduma za elimu, afya, kilimo na maeneo mengine yenye uhitaji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Januari 08, 2025, Makamu Mwenyekiti Bara wa chama hicho, Isihaka Mchinjita amesema mwaka 2024 haujatoa nafuu ya ugumu wa maisha huku kundi la vijana likiendelea kukosa ajira na shughuli za kueleweka za kujiingizia kipato.

“Aidha, tunaona sekta zinazopaswa kupewa kipaumbele ili ziweze kuajiri vijana wengi zinatelekezwa. tatizo la ajira halionekani kushughulikiwa na serikali ya CCM,” amesema mchinjita.

Advertisement

Mchinjita amesema jambo jingine linaloonesha hali ngumu ya maisha ni gharama za matibabu pamoja na ukosekana kwa mfumo rasmi wa kuwawezesha wananchi, pia mikopo umiza imekuwa changamoto kubwa kwa wananchi wanyonge, hasa wale wa kipato cha chini.