ACT yaongeza muda kuchukua, kurejesha fomu uchaguzi mkuu

CHAMA cha ACT – Wazalendo kimeongeza muda wa kuchukuwa na kurejesha fomu za kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.

Nafasi zingine ni ubunge, ubunge wa viti maalum, uwakilishi, uwakilishi wa viti maalum, udiwani na udiwani wa viti maalum.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Aprili 18, 2025, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema muda wa kuchukuwa na kurejesha fomu ya urais, Bara na Zanzibar ni kuanzia Aprili 18 hadi Mei 25, 2025.

Aidha, nafasi ya ubunge, ubunge viti maalum, uwakilishi na uwakilishi viti maalum ni kuanzia Aprili 18 hadi Mei, 31 2025 na udiwani na udiwani viti maalum ni kuanzia Aprili 18 hadi Mei 25,2025.

Ado amesema hatua hiyo ni kutekeleza maelekezo ya Kamati ya Uongozi Taifa ya Chama hicho iliyoketi katika kikao chake  Aprili 15, 2025 na kuielekeza Ofisi ya Katibu Mkuu kuongeza muda wa wanachama kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi hizo tajwa.

“Katika utekelezaji wa agizo la kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha tarehe 23 Februari 2025,Ofisi ya Katibu Mkuu ilitoa maelekezo ya kuruhusu wanachama kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali,”

Licha ya maelekezo hayo kutolewa kabla ya tamko rasmi la Chama cha ACT Wazalendo kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu 2025, wanachama wetu wengi wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali. Mathalani, kwa nafasi za ubunge, jumla ya wanachama 317 wamechukua fomu hadi sasa,”

Kwa nafasi ya uwakilishi, jumla ya wanachama 106wamejitokezakuchukua fomu. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wanachama wetuwaliojitokezakuchukua fomu. Kuchukua kwao fomu kabla ya chama kutangaza ushiriki kwenyeuchaguzi niishara ya wazi ya utayari wao katika mapambano ya kulinda na kutetea thamani yakura. Ninapenda pia kuwasisitiza wanachama ambao hawajachukua fomu watumie fursahii yasasakuchukua,” ameeleza Ado.

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button