ADDIS ABABA : MATAIFA 55 ya Umoja wa Afrika yatakutana Ijumaa mjini Addis Ababa kwa ajili ya kumchagua mwenyekiti mpya, huku mkutano huu ukiwa na changamoto za mzozo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na uamuzi wa Marekani wa kuondoa misaada ya kibinadamu kwa baadhi ya nchi.
Kusanyiko hili linatarajiwa kuwa na mjadala mzito, likikusanya wakuu wa mataifa ya Umoja wa Afrika unaohusisha karibu watu bilioni 1.5. SOMA: ‘Umoja wa Afrika usaidie kumaliza ugaidi EAC’
Kabla ya mkutano mkuu, viongozi hao watafanya kikao cha dharura kujadili machafuko yanayoendelea nchini Congo, ambapo waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameyakamata maeneo muhimu baada ya kushinda majeshi ya serikali.
Kwa mujibu wa Umoja wa Afrika, wakuu wote wa mataifa watahudhuria mkutano huu, ingawa haijulikani kama Rais wa Rwanda, Paul Kagame, atakutana ana kwa ana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi.