Afrika nzima nyuma ya Morocco

SAFARI iliyojaa matumaini mengi, licha ya ugumu wa kundi F, hawakusita kutumia saa sita na takribani mita 5,680 ambazo sawa na Miles 3,529 kutoka Morocco mpaka Qatar. Afrika inasubiri, Kiongozi wao wa juu, Waziri Mkuu, Aziz Akhannouch anasubiri kuona kama Morocco italinda historia ya mwaka 1986.

Bara la Afrika lina hamu kubwa ya kuona kama Morocco, itaungana na Senegal kwenda katika katua ya 16 bora ya mashindano ya Kombe la Dunia, ambapo saa 12:00 jioni ya leo atakipiga dhidi ya Canada Uwanja wa Al Thumama.

Kwa mara ya kwanza taifa hilo lilicheza mashindao hayo mwaka 1970 na kuishia makundi, halikupata nafasi tena hadi mwaka 1986 ambapo iliishia hatua ya 16, ambayo leo kwa mara nyingine itapigana kuirudia historia hiyo bora kuwahi kuiweka.

Katika kundi F, Morocco alipangiwa na timu za Poland, Portugal na England, lakini Morocco ilionyesha maajabu katika ardhi ya Mexico kwa kumaliza kundi hilo akiwa na pointi nne, nyuma ya England na Poland waliokuwa na tatu na Portugal mbili.

Bao la Lothar Matthäus, kiungo wa zamani wa Ujerumani na Bayern Munchen liliwaondoa kwenye mashindano Morocco na safari yao ya matumaini kuishia hapo, hata hivyo walitengeneza historia ambayo leo huenda ikajirudia.

Mwaka 1994 na 1998, walifuzu tena kwa bahati mbaya waliishia, makundi, hawakufuzu tena mpaka 2018 ambapo pia waliondolewa kwenye makundi. Afrika inaangalia, Morocco inaangalia, ni vita ya dakika 90.

Msimamo wa kundi F unaonyesha, Croatia ana pointi nne, sawa na Morocco tofauti ikiwa ni mabao ya kufunga na kufungwa, Belgium wana tatu, na Canada ambaye kimahesabu ameshatoka hana pointi yoyote.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x