Ajali yaua wafanyakazi wa Tanesco Ileje

WAFANYAKAZI wawili wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilayani Ileje mkoani Songwe, wamekufa na wengine 16 kujeruhiwa katika ajali na gari wakiwa kazini.

Mkuu wa wilaya hiyo, Anna Gidarya alisema ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia Novemba 2, mwaka huu baada ya gari walilokuwa wakisafiria kufeli breki, likaacha njia likiwa kwenye mwendo mkali kwenye mteremko na kutumbukia katika daraja la Mto Mwati.

Gidary alisema ajali hiyo ilitokea Kijiji cha Shuba, Kata ya Ibaba na wakati wa ajali gari hilo Dayada lenye namba za usajili SU 38133, lilikuwa na wafanyakazi 18.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Ileje, Joyce Ongati alisema wamepokea miili miwili na majeruhi 16.

Ongati alitaja majina ya waliokufa kuwa ni Juma Mbelwa (29) na Kanut Msafiri (32) na akasema majeruhi 14 ni wanaume na wanawake wawili na wote wametambuliwa ni wafanyakazi wa Tanesco.

Alisema majeruhi wawili walipewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Kanda ya Mbeya na wawili Hospitali ya Vwawa wilayani Mbozi kwa matibabu zaidi.

Habari Zifananazo

Back to top button