Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ahukumiwa miaka 20 Jela
ARUSHA: Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imemuhukumu kifungo cha miaka ishirini jela aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk John Marco Pima na wenzake wawili.
–
Akisoma hukumu hiyo Hakimu .Seraphin Nsana amesema Dkt pima na wenzake Mahakama imewakuta na hatia ya makosa tisa katika kesi uhujumu uchumi.
–
Kesi hiyo namba tano ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022 na kesi zingine zinazo wakabili bado hazijatolewa maamuzi.