MANYARA: KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Ally Hapi, amewataka vyama vya upinzani kuacha visingizio na kuogopa kushiriki uchaguzi, akisisitiza kuwa kazi kubwa zilizotekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan zinatosha kuipa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ushindi wa kishindo.
Akizungumza na wanaccm wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara ikiwa baada ya kuwasili kwaajili ya ziara ya siku nne mkoani humo, Hapi amebainikuwa maendeleo yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia ni dhahiri na hayahitaji propaganda za kisiasa.
“Tumeshuhudia miradi mikubwa ya maendeleo, kuboreshwa kwa huduma za kijamii, na uimarishaji wa uchumi. Wale wanaotafuta visingizio vya kukwepa uchaguzi wanapaswa kujitathmini badala ya kulaumu mfumo,” amesema.
SOMA ZAIDI: Rais Samia “msiwaogope wapinzani”
Aliongeza kuwa CCM itaendelea kuaminika kwa Watanzania kutokana na utekelezaji wa Ilani yake kwa vitendo, huku akiwataka wanachama wa chama hicho kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu mafanikio hayo.
Kauli ya Hapi inakuja wakati vyama vya upinzani vikidai kuwepo kwa mazingira yasiyo sawa katika uchaguzi. Hivyo ametaka vyama vya upinzani hususani Chadema kutokimbia uchaguzi maendeleo yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia yanatoa msingi imara wa ushindi wa chama hicho katika chaguzi zijazo.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Manyara James Darabe na Katibu Wazazi mkoa Manyara Christina Masagasi wameeleza kwamba ziara hiyo ni kielelezo cha uongozi bora katika CCM na jumuiya zake.
“Hapa ni utekelezaji wa ilani ya CCM kwakuwa shida na maendeleo ya nchi yanayotekelezwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan yanaelezwa kwa vitendo kuanzia ngazi ya shina,tawi na Taifa,tunapongeza utekelezaji huu wa ilani,”amesema Darabe.
Katika ziara hiyo Karibu Mkuu Wazazi Taifa amefanya mikutano ya hadhara kwa mabalozi,kuweka jiwe la msingi nyumba ya watumishi na kupanda miti