Amani yatajwa nguzo ya maendeleo ya taifa

MWANZA: VIJANA nchini wameombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kupiga kura, huku wakisisitizwa kudumisha amani ambayo imekuwa nguzo ya maendeleo ya taifa.

Haya yamebainishwa na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, katika kongamano la vijana lililofanyika jana.

Amesisitiza kuwa Tanzania ni kivutio cha wivu kwa watu wa mataifa mengine, kutokana na amani na utulivu iliyonayo.

Naye, Kashinde Paul kutoka Geita amesema vijana ni muhimu kushiriki uchaguzi kwa lengo la kuchagua viongozi wa taifa letu.

Amewaomba vijana wasijaribu kupoteza amani ya Tanzania na ni jukumu la kila kijana kulinda na kudumisha amani.

Naye Pendo Mlida kutoka mkoa wa Mara, amesema kuwepo kwa Uchaguzi Mkuu ni kiashiria kikubwa kuwa nchi yetu ya Tanzania ina Demokrasia

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button