Amuua mdogo wake kisa ugali

KENYA: REUBEN Lutabony ,42, ambaye ni mkazi wa Kilimani, Kaunti ya Kakamega nchini Kenya anatuhumiwa kumuua mdogo wake anayefahamika kwa jina la Michael Lukala ,40, baada ya kuzuka ugomvi baina yao uliohusisha ukubwa wa ugali waliokuwa wakiupika wote jikoni kwa mama yao.

SOMA ZAIDI: Auawa kwenye baa yake kwa wivu wa mapenzi

Kwa mujibu wa kaka yao mkubwa, Peter Lukala amesema wadogo zake waliingia kwenye mzozo huo wakati wakipika ugali baada ya kutoka kwenye kazi ya kuchimba kisima, ambapo Reuben anadaiwa alichukua shoka na kumshambulia mdogo wake Michael, hali iliyosababisha kifo chake.

Mama mzazi wa Michael na Reuben amesema alijaribu kuingilia kati ugomvi huo, lakini alizidiwa nguvu na Reuben, Jeshi la Polisi Kenya tayari linamshikilia Lutabony kwa ajili ya upelelezi zaidi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button