Asafirisha nyoka zaidi ya 100 kwenye suruali

RAIA mmoja wa China amekamatwa akisafirisha kimagendo nyoka 104 kwa kuficha kwenye suruali yake.

Taarifa ya Idara ya Forodha ya China imesema msafiri huyo ambaye hajatajwa jina amekamatwa na maafisa forodha wakati akijaribu kuvuka kutoka Hong Kong kuingia mpaka wa jji la Shenzhen, China.

Soma Hapa:http://CCM yamlilia Rais wa zamani wa China

Baada ya kumfanyia uchungzi wa kina, maafisa hao wamegundua akiwa na mifuko midogo sita yenye nyoka hao ameficha kwenye mifuko ya suruali.

Mifuko hiyo iliyokuwa imefungwa vizuri kwa utepe ilikuwa imehifadhi nyoka hai wa aina tofauti za umbo, ukubwa na rangi.

Habari Zifananazo

Back to top button