Ataka fidia Sh milioni 123 kupiga wimbo kwenye matangazo

Msanii wa Kizazi kipya, Nuni Suleimani (35) ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arusha kuiamuru Kampuni ya Mabasi ya Kilimanjaro Track kumlipa fidia ya Sh 123 baada ya kampuni hiyo kutumia wimbo yake wake kwenye matangazo ya biashara bila ruhusa yake.

Suleimani ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ya madai namba 36 mwaka 2022, alisema hayo mbele hakimu mwandamizi Wilaya ya Arusha, Bitony  Mwakisu na kudai kuwa kampuni hiyo ya imejinufaisha kwa kutumia wimbo wake wa Tabasamu Tanzania kujitangaza kibiashara.

Advertisement

Alidai hayo wakati akiongozwa na wakili wake, Lillian Justo akidai alianza kazi ya usanii wa nyimbo mwaka 2015 na nyimbo hiyo ya Tabasamu Tanzania aliikamilisha na kuiachia kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari mwaka 2021 na baadaye alikabidhiwa cheti cha umiliki wa wimbo kupitia Chama Cha Hakimiliki (COSOTA).

“Nipo mahakamani hapa kuiomba mahakama kuiamuru kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Track Co.Ltd kunilipa fidia  ya Sh  milioni 123 baada ya kutumia wimbo wangu kwenye matangazo yake ya biashara bila kunishirikisha. ”

Wakili Lilian alimuomba mteja wake kuvitambua baadhi ya vielelezo ikiwemo flash iliyokuwa na wimbo huo pamoja na cheti cha COSOTA na kuviwakilisha mahakamani ili vitumike kama vielelezo.

Mahakama ilipokea vielelezo hivyo baada ya wakili kwa mujibu maombi Godluck Michael kudai hana pingamizi na baadaye  wimbo huo ulikuwa kwenye flash ilichezwa mahakamani hapo kupitia runinga kubwa iliyokuwepo ndani ya mahakamani.

“Niliona nyimbo yangu inatumiwa kutangaza biashara  zinazotolewa na kampuni hiyo ya Kilimanjaro ,niliirekodi kupitia simu yangu ya mkononi na baadaye nilipeleka malalamiko yangu COSOTA”

Anaeleza kwamba COSOTA iliandika barua ya wito kwa kampuni ya Kilimanjaro lakini baada ya kukutana katika ofisi hizo za COSOTA huku kampuni hiyo ikiwakilishwa na kondakta wake ,hawakufikia mwafaka.

“Niliamua kuiandikia barua kampuni hiyo ( Demand Note) ya kusudio la kuishitaki nikitaka inilipe Sh milioni 123 ndani ya siku 14,hata hivyo hawakujibu chochote na baada ya muda huo niliamua kuja hapa mahakamani kudai haki yangu”

Akihojiwa na wakili, Lilian kuhusu uhalali wa akaunti hiyo na kampuni hiyo ,alisema alijiridhisha kuwa akaunti hiyo inamilikiwa na kampuni hiyo kutokana na kwamba  mawasiliano ya simu zote katika vituo vyote vya mabasi hayo nchini yalikuwa yameweka humo.

Nuni pia alidai mahakamani hapo kuwa  siku moja baada ya kampuni hiyo kupelekewa barua ya wito COSOTA tangazo hilo liliondolewa mtandaoni na pia uongozi wa kampuni hiyo haujawahi kujitokeza hadharani kukanusha kuwa akaunti hiyo sio mali yao na anwani zote zipo na vituo vya mabasi viliondoshwa katika akaunti hiyo.

Akihojiwa maswali ya dodoso na wakili anayeiwakilisha kampuni ya Kilimanjaro Track co.ltd , Goodluck Michael kama kweli ameiona wimbo wake mahakama ama ameona tangazo  Nuni alidai ameisikia ikiwa kwenye tangazo la biashara la kampuni ya Kilimanjaro.

Hakimu Mwakisu aliahirisha kesi hiyo hadi septemba 9 mwaka huu ambapo upande wa mashtaka utaendelea na shahidi mwingine siku hiyo.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *