AU yahofia mgawanyiko DR Congo

 

ADDIS ABABA: UMOJA wa Afrika umeonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu mgawanyiko wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kufuatia waasi wa M23, wanaoungwa mkono na Rwanda, kuchukua udhibiti wa mji mwingine wa Bukavu.

Waasi hao tayari wanadhibiti mji wa Goma, ambao walimteka mwishoni mwa mwezi Januari. Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Bankole Adeoye, amesema Umoja huo hautaki kuona taifa hilo likigawanyika na kusisitiza kuwa ni muhimu kudumisha umoja wa DRC.

Advertisement

Adeoye ametoa wito wa kuondolewa kwa waasi wa M23 na wale wanaowaunga mkono katika miji yote ya DRC, ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege wa Goma. SOMA: Baraza la Usalama AU kujadili mzozo DR Congo

Mapigano yanayoendelea nchini DRC yanazidi kuzua wasiwasi kwa mataifa jirani na yale ya Magharibi, huku hofu ikiwa inaongezeka kuhusu kuenea kwa mzozo huu. Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, alisisitiza kuwa vita hivi lazima viweze kudhibitiwa ili visiweze kuzua mizozo ya kikanda.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *