Bajeti Tamisemi yapita

...yatakiwa kuondoa changamoto ya madawati

BUNGE a Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 yenye jumla ya shilingi Trilioni 9.1.

Kati ya fedha zilizoombwa, shilingi Trilioni 5.6 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida yanayojumuisha mishahara ambayo ni shilingi Trilioni 4.5, matumizi mengine shilingi Trilioni 1.06 na shilingi Trilioni 3.4 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Hata hivyo, wabunge licha ya kuipitisha bajeti hiyo wameitaka Tamisemi kushughulikia suala la madawati kwa Watoto na asiwepo mtoto anayekaa chini katika kipindi hiki ambacho Benki ya Dunia imetoa ripoti kuwa Tanzania imepiga hatua katika uchumi wake.

Akikazia hoja hiyo, Spika wa Bunge, Tulia Ackson alisema ni aibu kwa karne hii Watoto kukaa chini na kutaka suala hilo lishughulikiwe ipasavyo ili mtoto anapoenda kuanza darasa la kwanza basi akute madawati ya kutosha.

“Ifike mahali hizi hoja za uhaba wa madawati ziishe,haiwezekani mpaka karne hii Watoto wanakaa chini, Tamisemi shughulikieni kero hii, na pia mnapojenga majengo mazuri ya shule msisahau kukarabati ya zamani, ifike mahali bunge hili liwe linajadili hoja kubwa kubwa tu sio kero za madawati, haipendezi..”Amesema

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button