Bandari Saccos yaboresha utendaji kazi

DAR-ES-SALAAM : MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari nchini imesema Chama cha Ushirika cha Kuweka na kukopa cha mamlaka hiyo kimesaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa Mamlaka hiyo na kupata nguvu ya kuhudumia mizigo inayofika katika bandari hiyo na kukuza uchumi wa nchi.

Akifungua mkutano mkuu wa 56 wa Chama cha Akiba na kukopa cha Bandarini, Mkurugenzi wa rasilimali watu wa mamlaka  ya bandari ,Musa Mzenga amesema kupitia Saccoss hiyo watumishi wameweza kukopa fedha na kujiendeleza kiuchumi.

“Ushirika ni dhana muhimu ya kujenga undugu,ujamaa na uchumi wa pamoja katika kuondoa umasikini,saccoss hii imekuwa na mchango chanya kwenye mamlaka ya bandari kwa kuwahudumia watumishi wake na kuwasaidia kukuza kipato kilichoongeza ufanisi wa utendaji kazi kwenye mamlaka hiyo kwa ufanisi na kukuza uchumi wa nchi kwa Ujumla.”alisema Mzenga

Advertisement

Mzenga aliongeza kuwa “Tumekuwa tukitoa ushirikiano na mazingira wezeshi ya kuhakikisha chombo hicho kinafanya kazi zake vizuri kwa kuzingatia ustawi wa watumishi na Taifa  kwa ujumla na kufanikisha jitihada za kuhudumia mizigo mingi inayofika katika bandari hoyo kuelekea katika maineo mbalimbali ndani na nje ya nchi.”

“Nimetaarifiwa kuwa kuna ushindani baina ywnu na taasisi zingine kama hii yenu ya kutoa kikopo,ninataka niwahakikishie nyie mnafursa kubwa ya kufanya vizuri kwenye mazingira ya ushindani kwa kuboresha huduma zenu mnazitoa kikubwa mfanye kazi kwa weledi na kuzingatia sheria za nchi na sheria za vyama vya ushirika”alisema Mzenga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Bandarini Saccos,Ernest Nyambo alisema alisema Saccoss hiyo imejipambanua zaidi kwenye ufanyaji kazi kwa kutumia teknolojia kwa kuweka huduma za fedha kigangani.

“Kwa hiyo Bandarini Saccoss ni moja ya taasisi kubwa,tunakwenda kujikita kuboresha miundombinu ya teknolojia ya TEHAMA,ili kusudi kuweza kumuhudumia mwanachama wetu hata aliyeko ukerewe,aliyeko kimondo,hana haja ya kufika ofisini”alisema Nyambo

Mrajisi msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa wa Dar es salaam,Anjella Malimi alitoa wito kwa vyama vya ushirika nchini kuendelea kufuata sheria na kanuni za vyama vya ushirika ili kuweza kuwahudumia wanachama kwa weledi na kuwaletea maendeleo.

“Saccos ikifuata sheria lazima ifanye vizuri na ikifanya vizuri lazima wanachama watakiwa na maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

SOMA: Bandari Mtwara yaendelea kuhudumia mizigo

Mikutano mikuu kwenye vyama ndio mahali ambapowanachama wanapanga mipango,kupitisha bajeti lakini wanaangalia taarifa za ukaguzi kama chama kimekaguliwa na kuweza kufanya uchagizi wa viongozi wao .

Mkutano mkuu wa Saccoss hiyo ulitanguliwa na shughuli za kurejesha faida waliyoipata kwa jamii kwa kuwanunulia miguu ya bandia wanafunzi walemavu wa shule ya Jesji la wokovu na wailes na kuchangia damu kwenye hospitali ya Rufaa ya Temeke.