Bandari Tanga yavutia wakulima Gairo
Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4720
MOROGORO; Wakulima wa Wilaya ya Gairo wamechagua bandari ya Tanga, kama bandari ya kimkakati kusafirisha mazao yote ya kilimo kwenda nchi mbalimbali kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa katika bandari hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Jabiri Makame wakati alipotembelea banda la bandari ya Tanga katika maonesho ya wakulima Nanenane Kanda ya Mashariki yanayofanyika viwanja vya Julius Nyerere mkoani Morogoro.
Amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani, ikiwemo kununua vifaa vingi na vya kisasa vya kupakia na kupakua mizigo, umemshawishi kuona bandari ya Tanga kuwa tegemeo la wakulima wa Wilaya ya Gairo kupitisha mazao yao ya kilimo.
Soma pia:‘Bandari Tanga kuwa ya kimkakati’
Kwa upande wake Ofisa Mipango wa Bandari ya Tanga,Tumgonze Kabigumila, amesema kwa sasa bandari ya Tanga ina uwezo wa kupokea meli kubwa yoyote, kwani ina kina kirefu cha mita 13 na tangu kukabidhiwa mradi huo bandari imehudumia meli kubwa 35.
Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4720