Bandari ya kusafirisha bidhaa chafu kujengwa 2025

UJENZI wa bandari ya kusafirisha bidhaa chafu eneo la Kisiwa Mgao mkoani Mtwara unatarajiwa kuanza mwezi Januari mwaka 2025, Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa anaeleza.

Waziri Mbarawa amesema hayo leo  mara baada ya kutembelea kukagua eneo la ujenzi wa bandari hiyo.

“Mkandarasi ameshapatika tutamkabidhi mradi mwezi Januari mwakani ili aanze kazi,” amesema.

Advertisement

Mbarawa amesema mradi huo wenye thamani ya Sh bilioni 434 utajengwa kwa miezi 30 na kumalizika ifikapo Juni mwaka 2027.

Waziri amesema serikali imejipanga kuhakikisha mradi unajengwa na kukamilika kwa wakati ili uweze kufanya kazi kama ilivyopangwa.

“Sisi kama serikali tumejipanga kuhakikisha kwamba fedha kwa ajili ya mradi zinatolewa wakati wote zitakapokuwa zinahitajika ili kumaliza kazi ya ujenzi bila kuchelewa,” amesema.