Barcelona kukiwasha ugenini LaLiga leo
BAADA ya kukusanya pointi 6 katika michezo miwili ya mwanzo ya Ligi Kuu ya Hispania-LaLiga miamba ya soka Barcelona inashuka uwanja wa ugenini leo kuivaa Rayo Vallecano.
Mchezo huo utafanyika uwanja wa Campo de Futbol de Vallecas uliopo Madrid.
SOMA: Laliga kuanza kutimua vumbi leo
Barcelona inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa LaLiga ikiwa na pointi 6 baada ya michezo 2 wakati Rayo Vallecano ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 4.
Katika mchezo mwingine wa LaLiga, Mallorca itakuwa mwenyeji wa Sevilla kwenye uwanja wa Mallorca Son Moix.
Sevilla inashika nafasiya 14 ikiwa na pointi 1 baada ya michezo 2 wakati Mallorca ipo nafasi ya 16 pia ikiwa na pointi 1.