Barcelona yageukia kwa Kingsley Coman

TETESI za usajili zinasema klabu ya Barcelona imeelekeza nia yake ya usajili kwa winga wa Bayern Munich, Kingsley Coman baada ya kushindwa majaribio kupata saini ya Nico Williams kutoka Athletic Club. (El Nacional – Spain)

Napoli imefungua mazungumzo na Manchester United kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa Scotland, Scott McTominay, 27, na ingependelea dili la mkopo. (Times – subscription required)

SOMA: Napoli yakanusha kumdhihaki Osimhem

Pia Napoli inakaribia kumsajili kiungo wa Scotland, Billy Gilmour, 23, kutoka klabu ya Brighton & Hove Albion. (Corriere dello Sport – in Italian)

Mshambuliaji wa Napoli na Nigeria, Victor Osimhen.

Chelsea imerejea katika mazungumzo na Napoli kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Nigeria, Victor Osimhen,25. (Talksport)

Paris Saint-Germain imeanza kupunguza nia yake ya kumsajili winga wa Manchester United, Jadon Sancho,24, na sasa inafikiria kujiondoa katika mbio za kumsajili Osimhen.

Winga wa Manchester United aliyeko Borussia Dormund kwa mkopo, Jadon Sancho.

West Ham United inapanga dili kumsajili Tammy Abraham,26, wa timu ya Roma huku klabu hiyo ya Serie A ikikusudia kumuuza mshambuliaji huyo kwa pauni milioni 25. (Gazzetta dello Sport via Football Italia)

Habari Zifananazo

Back to top button