Napoli yakanusha kumdhihaki Osimhem

KLABU ya Napoli imesema video iliyopostiwa Septemba 26,2023 kupitia ukurasa wa Tiktok wa klabu hiyo ikionesha kumkejeli, mshambuliaji, Victor Osimhen haikuwa na lengo la kumdhihaki.

Jana Septemba 27, 2023, Mnaigeria huyo akiwakilishwa na wakala wake walitishia kuishtaki klabu hiyo kwa kitendo hicho ambacho kimetafsiriwa kama dhihaki na kumkosea heshima nyota huyo.

Napoli wamesema: “Kwa vyovyote vile, ikiwa Victor angeona kosa lolote kwake, hii haikuwa kile klabu ilikusudia”.

Advertisement

“Calcio Napoli, wanaotaka kukwepa unyonyaji wowote wa suala hilo, wanaeleza kwamba hatukuwahi kutaka kumuudhi au kumkejeli Victor Osimhen, ambaye ni hazina ya klabu hii.

” imeeleza Napoli.

“Mitandao ya kijamii, haswa TikTok, daima imekuwa ikitumia aina ya lugha ya kujieleza yenye moyo mwepesi na ubunifu, bila kutaka, kama ilivyo kwa Osimhen kama mhusika mkuu, kuwa na nia yoyote ya matusi au dhihaka”.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *