Barcelona yamsajili Wojciech Szczęsny

KLABU ya Barcelona na Wojciech Szczęsny wamefikia makubaliano golikipa huyo kujiunga na timu hiyo hadi Juni 30, 2025.

Barcelona imetangaza makubaliano hayo kupitia vyombo vyake vya habari.

SOMA: Barcelona kukiwasha ugenini LaLiga leo

Szczęsny mwenye umri wa miaka 34 alianza kucheza klabu ya Legia Warsaw ya Poland akiwa na umri wa miaka 16 kabla ya kujiunga na Arsenal Januari 2006 ambako alianza michezo ya kulipwa 2009.

Timu nyingine alizocheza ni Roma na Juventus za Italia .

Akiwa timu ya taifa amecheza mechi 84 akishiriki mashindano mawili ya Kombe la Dunia na manne ya Kombe la Ulaya.

Kwa jumla Szczęsny amecheza zaidi ya michezo 500 za kulipwa, 75 zikiwa za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Habari Zifananazo

Back to top button