Benki ya AIIB kutoa dola bilion 1.5 upatikanaji umeme Afrika

RAIS wa Benki ya Asia Infrastructure Investment Bank (AIIB), Jin Liqun ameahidi benki hiyo itatoa Dola Bilioni 1.5 kuunga mkono upatikanaji wa umeme kwa watu milioni 300 Afrika ifikapo 2030.
Ahadi hiyo ametoa leo Januari 27, 2025 ikiwa siku ya kwanza ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.



