MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Murtallah Mbillu ametekeleza agizo la Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa kwa kuwajengea kituo cha waendesha bodaboda eneo la Wasso wilayani humo.
Mbillu amesema agizo la Waziri Mchengerwa amelitekeleza kwa vitendo kwa kuwajengea maofisa usafirishaji (bodaboda) maeneo ya kujiegesha ili kuwawekea mazingira bora ya kazi.
“Tumewajengea bodaboda kituo ili kujikinga na mvua na vituo vingine viwili vitajengwa ili kuwezesha vijana hao kufanya shughuli zao za kujikwamua kiuchumi na natoa rai Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 26 mwaka huu wajitoteze kujiandikisha kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kupigia kura,” Mbillu.
SOMA: Mchengerwa: Wakurugenzi jengeni vituo vya bodaboda
Pia amewatakawale wenye sifa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kujitokeza kuwania nafasi hizo.
Emmanuel Thomas anayejihusisha na bodaboda ameshukuru kujengwa kituo hicho ambacho kitawasaidia kujikinga na jua pamoja na mvua wakati wakitafuta riziki zao na kuomba vituo vingine viendelee kujengwa.
SOMA: Ajali za bodaboda bado tishio
Wakati huo huo kiongozi wa waendesha bodaboda hao ,Lwage Pemba amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutengeneza mazingira bora ya kufanyia kazi kwa wakazi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Wasso Loliondo.
Awali Waziri Mchengerwa alitoa maagizo kwa halamshauri zote nchini kuwajengea maofisa usafirishaji vituo vya kuegesha vyombo vyao vya moto.
View this post on Instagram