Bossi FBI: Msijibu ’emails’ za Musk

WASHINGTON: MKURUGENZI mpya wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), Kash Patel amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kutojibu barua pepe ‘email’ kuhusiana na utendaji kazi wao wa kila wiki kama ilivyoelekezwa na Elon Musk.
Elon Musk ambaye ni Msimamizi wa Idara ya Ufanisi wa Serikali (Doge) chini ya uongozi wa Rais wa Marekani, Donald Trump aliagiza wafanyakazi wote nchini humo kuwasilisha ripoti ya utendaji kazi wao wa kila wiki kupitia ‘email’ ya Usimamizi wa Wafanyakazi (OPM), nchini humo.
Kutokana na amri hiyo, maelfu ya wafanyakazi katika Serikali ya shirikisho (Federal Goverment) walipewa saa 48 tu kuwasilisha ripoti ya utendaji kazi wao kwenda OPM hali iliyozua sintofahamu.
Hata hivyo, Patel ambaye alithibitishwa na Seneti Alhamisi, jana Jumapili amepinga ombi hilo. FBI ilikuwa inasubiri mwongozo wa ziada kutoka Wizara ya Sheria kuhusu hatua zinazofuata kwenye ombi hilo.
Chanzo: ABC News



