Boti yapinduka yaua watumishi 6 Kigoma

KIGOMA; WATUMISHI sita wa Idara ya Afya halmashauri ya Wilaya Kigoma mkoani Kigoma wamekufa, baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kutoka Kigoma Mjini kuelekea Kijiji cha Kagunga, Halmashauri ya Wilaya Kigoma kwa shughuli ya kutoa chanjo kukumbwa na dhoruba Ziwa Tanganyika na kupinduka.

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa Kigoma, Michael Maganga alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili asubuhi leo Machi 13, 2026 Kijiji cha Kalalangabo Manispaa ya Kigoma Ujiji na kwamba miili hiyo sita imepatikana.

Taarifa za awali ambazo Daily News Digital ilizipata mapema leo na kuzisambaza kutoka eneo la tukio zilisema mtumbwi ulipinduka na kuua watumishi hao, lakini kwa mujibu wa Maganga iliyopinduka ni boti.

Maganga amesema watu wengine tisa ambao pia walikuwa kwenye boti hiyo wameokolewa na kwa sasa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kigoma Maweni, huku juhudi za kutafuta watu watatu walikuwa pia kwenye boti zikiendelea.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button