DAR ES SALAAM: WAZIRI wa viwanda na biashara Dk, Ashatu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye jukwaa lililoandaliwa na Kampuni ya Jadore Couture yenye lengo la kuchangisha sare za wanafunzi 5000 wanaoishi mazingira magumu.
Jukwaa hilo litaonesha bunifu mbalimbali za mavazi ya wakina mama na fedha zitakazopatikana zitasaidia kwenye upatikanaji wa sare hizo.
Hayo ameyasema Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Jadore Couture Ruth Urio Desemba 11,2023 Jijini Dar es salaam. Ameongezea kwa kusema wanatambua dhahiri wanafunzi wanaoishi maisha magumu hivyo ni vyema kuwapa tabasamu kwa kuungana naserikali ya awamu ya tano
Kwa upande mwingine ameongezea kwa kusema kutakuwa na wasanii mbalimbali pamoja na wadau watakaoshiriki katika jukwaa hilo pia amesema wanamatarajio ya kwenda mikoa mingine hivyo wameanza na Mkoa wa Dar es salaam na kila mwaka wamekuwa wakichangisha sare hizo.
Jukwaa hilo linatarajiwa kufanyika Jijini Dar es salaam, Desemba16, 2023