DAR-ES-SALAAM : WANAMUZIKI wakongwe wa Tanzania wanazidi kuaga dunia na kuacha ombwe kwenye muziki wa dansi wa asili, na leo kinachoendelea ni msiba wa gwiji King Kikii
King Kikii ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 77, akiacha alama kubwa – sauti yake – ambapo aliendelea kuimba hadi akiwa na uzee wake.
Simanzi imetawala ghafla katika mioyo ya mashabiki wa muziki wa dansi, huku utandu mweusi ukiwa umetanda.
Msiba huu huwezi ukazungumza wala kuuelezea imebaki tu kutafakari, nani ambaye atatupa tena vionjo vya muziki wa dansi nchini? Nani atakayebeba alama ya kutangaza lugha ya Kiswahili katika nyimbo za dansi? Ni maswali ambayo hayana majibu bado naendelea kutafakari.
Boniface Kikumbi maarufu kwa jina la kisanii ‘King Kikii’, amejizolea umaarufu mkubwa Tanzania kwa mchango wake wa muziki wa dansi.
Sauti yake ya kipekee iliyoonesha ufanisi mkubwa wa uandishi na uwezo wa kuchanganya mitindo mbalimbali ya muziki, King Kikii ameweza kujiimarisha kama mmoja wa wasanii wenye uwezo mkubwa wa muziki huo.
King Kikii alikulia katika mazingira ya familia inayothamini sana sanaa na muziki na hii ilimsaidia kuwa na shauku ya kuwa mwanamuziki tangu akiwa mdogo.
Safari yake ya muziki ilianzia akiwa mdogo, ambapo alianza utunzi wa muziki na kuanza kuimba akiwa angali mdogo. Waswahili wanasema kila mtu ana historia yake.
King Kikii ni msanii aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kuchanganya muziki wa kisasa ‘Bongo fleva, Afrobeat na pop na kuleta ladha tofauti ya uandishi na utunzi wa nyimbo.
Mchanganyiko huu wa beats za kisasa, mashairi ya kuvutia na sauti yake ya kipekee kulimfanya nguli huyu wa muziki kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa muziki wa kisasa kadhalika na watu wazima.
Alikuwa ni mtu aliyependa kuandika nyimbo zinazogusa masuala ya kijamii, upendo, changamoto za maisha, na hamu ya kufanikiwa.
King Kiki amepata umaarufu mkubwa kupitia vibao vyake mbalimbali vilivyovuma katika vituo vya redio na televisheni kama Nashukuru, Mwandishi, Zigo la Moyo bila ya kusahau Kitambaa Cheupe ni miongoni mwa nyimbo ambazo zilichangia kujenga jina lake kimuziki.
“Hallo mama naondoka ye, ye
Naenda nitarudi, nyuma wabaki jihadhari na watu, fitina na wambea hao,” sehemu ya mashairi ya wimbo Kitambaa Cheupe wa mwanamuziki King Kikii.
King Kikii alikuwa ni mtu aliyependa kutunza faragha na hahitaji kuzungumzia sana maisha yake binafsi kwenye vyombo vya habari.
Katika mahojiano mbalimbali alikuwa ni msanii aliyesisitiza kuwa mafanikio yake yametokana na kufanya kazi kwa bidii, kujitolea, na kuwa na mipango ya dhati.
King Kikii pia ameweza kuwa na mafanikio makubwa katika sekta ya biashara. Kwa kutumia umaarufu wake na uwezo wa kuzungumza na mashabiki kupitia muziki, alifanikiwa kutengeneza mkataba na baadhi ya kampuni za matangazo na kushirikiana na brand maarufu Tanzania.
Hii imekuwa faida kubwa kwa ajili ya kuongeza kipato chake na ushawishi wake katika sekta ya muziki na biashara.
Msanii huyo amekutana na changamoto nyingi katika safari yake ya muziki, kutoka kwa mashindano na ushindani wa wasanii wenzake hadi kutafuta nafasi za kimataifa.
Hata hivyo, alikabiliwa na changamoto hizi kwa umahiri na amekuwa mfano mzuri wa msanii anayependa kupanua upeo wake na kutafuta namna bora ya kuwa na ushawishi katika sekta ya muziki duniani.
Msanii huyo ameleta mabadiliko makubwa ya tasnia ya muziki wa kitanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Kupitia ufanisi wake wa kisanaa, amejizolea umaarufu na anaheshimika kama miongoni mwa wasanii wakongwe waliokuwa wakishirikishwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
Amepata tuzo mbalimbali ikiwemo msanii bora wa muziki wa dansi na mtunzi bora wa muziki katika kuendeleza lugha ya Kiswahili.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ambavyo amewahi kunukuliwa wakati wa uhai wake, vinaeleza kuwa King Kikii ambaye jina lake la asili ni Kikumbi Mwanza Mpango, alizaliwa Januari 01, 1947 katika mji wa Lubumbashi uliopo mkoa Katanga nchini Congo Belgium, ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), akiwa mtoto wa tano kuzaliwa kwa mama Katambo Wabando Paulino na Mwanza Jumban
Alianza masomo ya awali mwaka 1953 akiwa na umri wa miaka sita mjini Lubumbashi, baadaye baba yake alihamia katika mji wa Likwasi ambako aliendelea na elimu hiyo katika shule ya Officialle Laique de Kolwezi.
Alibuni njia za kujiendeleza kimuziki akawa anachukua ujuzi wa kucheza mitaani, akaupeleka shuleni ambako aliwatafuta wenzake watatu wakaanzisha kikundi cha muziki wa dansi wote wakiwa darasa la tano, wakiimba na kucheza hata walimu wao waliupenda muziki huo kila sherehe za shule waliitwa kutoa burudani.
Sifa za umahiri wao zikazagaa maeneo mengi ikizingatiwa kwamba walikuwa vijana wadogo wakifanya mambo makubwa na hapo ndipo safari yake kimuziki ilipoanzia kuanzia huko Congo hadi kuingia Tanzania.