Burkina Faso waiomba JKCI ujuzi matibabu ya moyo

DAR ES SALAAM: SERIKALI ya Burkina Faso kupitia washauri wa rais na madaktari bingwa, wamefika nchini Tanzania kuingia makubaliano ya kupata ujuzi wa matibabu ya magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk. Peter Kisenge amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema wajumbe hao wamefika nchini kutokana na taasisi hiyo kuwa moja ya taasisi kubwa barani Afrika katika tiba ya magonjwa ya moyo, hivyo wamekuja kwaajili ya kujifunza ili na wao wakaanzishe taasisi kama hiyo.

Kisenge amesema wamekubali kuleta watu wao kwa ajili ya mafunzo katika taasisi hiyo pia wamekubali kuleta wagonjwa wenye matatizo ya moyo ambao walikuwa wanawapeleka nchi za ulaya kwa ajili ya matibabu.

Advertisement

“Wamekubali kuleta watu wao katika taasisi yetu, lakini wamekubali kuleta wagonjwa wao waliokuwa wanawapeleka nchi za Ufaransa na uturuki kwa ajili ya kutibiwa, Rais wao amesema maendeleo ya Afrika yanajengwa na waafrika wenyewe,” amesema.

Aidha, amesema ushirikiano huo pia utailetea Tanzania faida za kiuchumi kupitia fedha za kigeni na kuongeza nafasi kwa nchi nyingine za Afrika kuleta wagonjwa wao kwa matibabu bora JKCI.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Burkina Faso, Adama Sawadogo,amesema ziara hiyo ni sehemu ya mpango wa kuboresha huduma za upasuaji wa magojwa ya moyo nchini kwao.

“Tunajivunia sana kile kinachofanyika hapa, JKCI ina viwango vya kimataifa, na hii ndiyo aina ya ubora tunaotaka kuiga nchini Burkina Faso.” Amesema Sawadogo.

Mratibu wa Utalii wa Matibabu wa Wizara ya Afya, Asha Mahita, Tanzania imekuwa ikifanya vizuri kwenye masuala ya Afya, hivyo kutokana na changamoto walizonazo nchini kwao wamekuja kufanya makubaliano ya kuboresha sekta ya afya.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *