CCK yaahidi mageuzi kwa wananchi

ARUSHA: CHAMA cha Kijamii (CCK) kimeishukuru Serikali kwa kutoa magari kwa kila mgombea kupitia Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) pamoja na kujenga nyumba na kugawa kwa wananchi kwa bei nafuu ili kila mmoja aweze kumiliki.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za urais wa chama hicho uliofanyika leo katika Soko Kuu la Jiji la Arusha, Mgombea Urais wa CCK, David Mwaijojele, amesema chama chake kimejipanga kuleta mageuzi makubwa yatakayowaondoa watanzania kwenye changamoto za maisha ya kila siku.
Mwaijojele amesema endapo chama hicho kitapata ridhaa ya kuongoza nchi, kitaweka mkazo kwenye kilimo cha kisasa na umwagiliaji ili kuongeza upatikanaji wa chakula na kuhakikisha wananchi wanapata milo mitatu kwa siku. SOMA: CCK kuunda serikali ya umoja wa kitaifa
Aliongeza kuwa CCK kimepanga kushusha gharama za matibabu kwa kufanya bima ya afya kupatikana kwa bei nafuu, pamoja na kushusha bei za vocha za simu, gesi na umeme ili wananchi wanufaike na rasilimali zao.



